LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 22, 2014

MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE SAIDI BWANAMDOGO KUMSUBIRI RAIS KIKWETE

MAREHEMU BWANAMDOGO
NA BASHIR NKOROMO, Pwani
MAZISHI ya Mbunge wa Chalinze mkoa wa Pwan, Saidi Mwanamdogo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho, katika Kijiji Cha Miono, Bagamoyo, sasa yatafanyika keshokutwa kutoa nafasi kwa Rais Jakaya Kikwete kuhudhuria mazishi hayo.
Mazishi hayo yatafanyika siku hiyo kutokana na kusubiriwa kwa Jakaya  Kikwete ambae yupo nchini Uholanzi katika ziara ya kikazi.
Akizungumzia leo  nyumbani kwa marehemu, Makondeko Dar es Salaam,  ambako ndipo msiba ulipo kwasasa kabla ya kusafirishwa ijumaa, asubuhi, Baba mdogo wa marehemu Omar Khalfan Nguya amesema baada ya Rais Kupata taarifa hizo nje ya nchi  ameomba siku ya kuzika iahirishwe na kufanyika ijumaa wiki hii.
Amesema Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kuanzishiwa matibabu nchini india ambapo kwa kudra za mwenyezi mungu mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Marehemu Said BwanaMdogo ameacha mjane na watoto sita huku wawili kati ya hao wakiwa ni wa nje ya ndoa.
Wakati huohuo, Katibu wa CCM Mkoani Pwani Sauda Mpambalioto amesema wamepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kukiri kubadilishwa kwa siku ya mazishi.
Mpambalioto amesema mbali ya msiba huo pia jana, wamemzika mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa MNEC kupitia Mkuranga, Rukia Ally Msumi ambae alipata ajali ya pikipiki ambayo ilisababisha kifo chake.
Nae mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema msiba huo ni pigo kwake kwani walikuwa karibu na marehemu kwa kushirikiana kikazi na kupeana mawazo ya kiutendaji.
Koka amesema Bwanamdogo alikuwa ni mtu mcheshi, msikivu ,asiye na majivuno ,alipenda kuzungumza na kila rika pasipo kuwa na majivuno hali inayomfanya awe na kitu cha kuiga kwake.
Amesema kutokana na sifa alizokuwana nazo marehemu haina budi akawa mfano wa kuigwa na wabunge wengine na kuwataka wabunge wote kwa pamoja kushikamana na kuwa kitu kimoja ili kujenga nyumba moja bila ya kubaguana .

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages