LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2014

HALI YA AFYA YA MHESHIMIWA RAIS, JAKAYA MRISHO KIKWETE YAENDELEA KUIMARIKA..

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazoezi ya kutembea baada ya kufanyiwa operesheni ya tezi dume katika hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani  


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.


Hali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alifanyiwa operesheni Jumamosi, inaendelea kuimarisha na kuwa nzuri na jana, Jumapili, Novemba 9, 2014, alianza kufanya mazoezi ya kutembea.

Rais Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya kufanyiwa operesheni ya tezi dume (prostrate) kwenye Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, itaendelea kuwapatia wananchi habari sahihi kuhusu maendeleo ya afya ya Mheshimiwa Kikwete kwa kadri habari hizo zitakavyokuwa zinapatikana.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kuwashukuru sana wote ambao wamekuwa wakimwombea Rais Kikwete, ili apone haraka na kurejea nyumbani kujiunga na wananchi wenzake katika ujenzi wa taifa letu. Tunawaomba waendelee kumwombea.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages