LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 28, 2015

RAIS ROBERT MUGABE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA VIONGOZI VIJANA WA AFRIKA NA CHINA

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika leo kwenye hotel ya Ngurdoto ,Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea tuzo ya Heshima ya kuhamasisha amani na utulivu barani Afrika kutoka kwa Rais wa Umoja wa Vijana wa Afrika uliochini ya Umoja wa Afrika (AU) Francine Furaha Muyumba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa waliohudhuria Kongamano la Tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika Ngurdoto,Arusha.
 Rais wa Umoja wa Vijana wa Afrika ulio chini ya Umoja wa Afrika Francine Furaha Muyumba akihutubia katika kongamano hilo.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (katikati) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)Stepehen Masele wakisikiliza hotuba ya Rais wa Umoja wa Vijana wa Afrika ulio chini ya Umoja wa Afrika Francine Furaha Muyumba

 Bendi ya Polisi ya Moshi (brass band) ikitumbuiza wakati wa Kongamano

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi mbali mbali wakati wa Kongamano.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui akiingia ukumbini akiongozana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)Stepehen Masele
 Baadhi ya wajumbe kutoka China
 Baadhi ya wajumbe wa kongamano

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika Kongamano la Tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika Ngurdoto,Arusha.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui akihutubia wakati wa Kongamano la Tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika Ngurdoto,Arusha.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(katikati) na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano wa Kongamano la Tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China lililofanyika Ngurdoto Arusha.
PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages