LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 9, 2015

MAGUFULI : GESI YA BAGAMOYO ITALINUFAISHA TAIFA

 
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini.

Hayo ameyasema leo wilayani Bagamoyo katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo amesema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali take.

"Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena imegunduliwa katika eneo la ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.

"Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania yote," amesema Dk. Magufuli
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo  jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
Mgombea ubunge wa jimbo  jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akimnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages